}

Ligi kuu Tanzania bara mzunguko wapili kuanza kutimua vumbi Desemba 17.

Na. Anaseli Stanley Macha.


Ratiba ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara imetangazwa rasmi leo hii ambapo ligi hiyo inataraji kuendelea tarehe 17 ya mwezi huu katika viwanja tofauti hapa nchini.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo,Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kwamba ratiba hiyo imezingatia michuano mbalimbali ili kuondoa upanguaji wa ratiba mara kwa mara.

Lucas amesema kwamba raundi ya 16 itachezwa tarehe 17 na 18 ambapo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam timu ya JKT RUVU itakuwa mwenyeji watakapoikaribisha Yanga, huku mechi nyingine itakuwa Mbeya City wakiwa  nyumbani watawakaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Ruvu Shooting itakuwa katika uwanja wa Mabatini ikiwakaribisha Mtibwa Sugar ya kule turiani mkoani morogoro, na mchezo mwingine utawakutanisha  Mwadui watakapowaarika Toto Africans mchezo utakao pigwa katika  uwanja wa Mwadui Complex huko mkoani shinyanga.

Raundi hiyo ya 16 inataraji kuendelea tena tarehe 18 katika viwanja tofauti ambapo wekundu wa Msimbazi watakuwa ugenini mkoani Mtwara kumenyana na Ndanda katika mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa Nangwanda.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.