}

Bodi ya Ligi yatoa ratiba Ligi ya vijana Chini ya miaka 20.

Na. Anaseli Stanley Macha.

Bodi ya ligi imetangaza ratiba ya michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 hatua ya nusu fainali ambapo michuano hiyo  inataraji kuendelea tarehe 9 ya mwezi huu katika uwanja wa Azam Complex ambapo nusu fainali ya kwanza itazikutanisha timu za simba na stand unitedi  mchezo utakaochezwa kuanzia mishale ya saa kumi jioni 

mchezo mwingine utakuwa kati ya Azam watakapo wakaribisha mtibwa sukar mchezo utakao pigwa katika majira ya saa moja usiku katika uwanja huo huo wa azam complex

Mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo unatarajiwa kupigwa tarehe 11 / 12 / 2016. ambapo timu zitakazo shindana katika hatua hiyo zinatarajiwa kuwa zile ambazo zitapoteza mchezo wao katika hatua ya nusu fainali

tamati ya michuano hiyo inatarajiwa kumalizika pia baada ya kupigwa  mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ambapo timu mbili zilizo shinda katika hatua ya nusu fainali zitakapo menyana katika hatua ya fainali ya michezo hiyo ambapo mchezo huo wa fainali uatnarajiwa kutimua vumbi mnamo saa moja usiku.

Pamoja na hayo shirikisho la soka tanzania TFF limesema kocha wa timu ya taifa ya vijana  serengeti boys bakari nyundo shime anaendelea kuwa kocha mkuu wa timu hiyo ingawa kwa sasa shime ni kocha wa klabu ya maafande wa JKT ruvu ya kule mkoani pwani .

Afisa habari wa shirikisho la soka tanzania TFF Alfred Lucas amesema kwamba wanaendelea kumtambua shime kama kocha wa serengeti boys kwa mujibu wa mkataba wao na kocha huyo ambao unamruhusu kocha shime kutoa huduma yake katika kikosi hicho pale timu inapokuwa kambini.

Aidha lucas amesema kwamba kikosi cha serengeti boys bado kipo ingwa kwa sasa wako katika maandalizi ya kikosi cha serenget boys ndogo chini ya miaka 14 ambayo nayo inatarajia kucheza michezo ya kirafiki katika mikoa mbalimbali na baadae kuja kutambumbulishwa rasmi kwa wadau wa soka kwa kucheza mchezo wa kimataifa wa dhidi ya shelisheli.

kocha Bakari nyundo shime mchawi mweusi hivi karibuni ameanza kazi ndani ya klabu ya JKT Ruvu ya kule mkoani pwani kwa kuwaeka wachezaji kambini akiongoza maanadalizi ya mzunguko wa pili ligi kuu tanzania bara ambapo anatarajiwa kuingia kandarasi iyopungua mwaka mmoja na nusu na maafande hao. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.