}

Al-shabaab waonja joto ya jiwe Somalia.

Idadi kubwa ya wanamgambo wa Al-shabaab wameyakimbia makazi yao baada ya mashambulizi ya Anga yanayodhaniwa kufanywa na wanajeshi wa Marekani.

Ndege zakivita za kigeni zimeripotiwa kuvamia kambi ya Al-shabaab inayojulikana kama Ibrahim Ali Berre iliyopo zaidi ya km 190 kaskazini magharib mwa mji mkuu Mogadishu.

Ripoti zinasema kuwa mashambulizi yalifanywa na askari wa Marekani kwakushirikiana na Majeshi ya Kenya (Kenya Defence Force KDF) Ikiwa ni mikakati yakuliangamiza kundi la Al-shabaab.

Kenya imekuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya ugaidi tangu ilipopokea ndege sita aina ya Bell Heuy II zenye thamani ya sh. Bilioni 11.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.