}

YANGA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA SINGIDA TAIFA

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Young Africans wameshindwa kutamba katika Uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Singida United jioni hii.

Singida United ndiyo walikuwa wa kwanza kupachika bao katika dakika ya pili tu ya mchezo kupitia kwa Kambale Salita.

Zikiwa zimeongezwa dakika 3 kuelekea mapumziko, Yanga walisawazisha bao hilo kupitia mpira wa adhabu ya kona uliopigwa na Ibrahim Ajibu na kumkuta beki Abdallah Shaibu ambaye bila ajizi aliutia kimiani kwa kichwa.

Matokeo hayo  yanaipa msala Yanga ambayo imerejesha tena pengo la utofauti wa alama 5 kati yake na Simba iliyo kileleni kwa kuwa na pointi 52.

Utofauti wa alama hizo unaiweka Yanga katika mazingira magumu ya mbio za kuwania ubingwa wa ligi kati yake na Simba ambayo ina njaa ya kutouchukua kwa takribani miaka mitano sasa. 

Sare hiyo imeifanya Yanga kujiongezea alama moja pekee kwa kufikisha 47, kwenye nafasi ya pili ya msimamo wa ligi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.