RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MWEYEKITI BODI YA TAIFA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Isaya Jayambo Jairo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Jairo unaanza leo tarehe 11 Aprili, 2018.
Prof. Jairo ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) na ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Aprili, 2018
No comments