}

TIRA IMEWAFUTIA LESENI KAMPUNI ZA USHAURI NA UDALALI WA BIMA.

Na. Happy Shirima-Dar. 
Mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima nchini (TIRA)imefutia leseni kampuni za USHAURI  na udalali was bima (insurance broker)kwa kukiuka utaratibu was uwendeshaji was biashara za bima.

Akizungumza jijini Dar es salaam kamishna wa bima Dkt Baghayo Saqware alisema kuwa Katika usimamizi wa solo la bima hapa nchini mamlaka hiyo imebaini ukikwaji was sheria ya bima namba 10 ya mwaka 2009 inayotoa taratibu za ufanyaji was biashara za bima kwa baadhi ya makampuni was udalali wa bima.

Akizitaja makampuni zilizofutiwa leseni  Dkt Saqware amesema kuwa Ni kampuni ya udalali wa bima ya HANS,  ENDEAVOUR, LEGEND OF EAST AFRICA na SWIFT  kwa kushindwa kuwasilisha tozo za bima  kwa makampuni ya bima hivyo kuwanyima wateja wa bima kupata haki ya kunufaika na fidia zao

Aidha ameongeza kuwa  pamoja na kuzifutia kampuni hizo pia wanashirikiana na mkurugenzi was upelelezi wa makosa ya jinai ili kuhakikisha kuwa wamiliki wa makampuni hayo wanapatikana na kuchukuliwa hatua za 

Kisheria  pia kwa ukwepaji wa ukaguzi wa mara kwa mara wa mamlaka ikiwa ni pamoja na kutokufungua ofisi zao.
Hata hivyo amewataka wananchi kutambua uwepo wa mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima nchini hivyo wasisite kuwasilisha malalamiko yao kwao ili hatua za Kisheria zifuatwe.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.