}

YANGA YAPEWA BINGWA WA MKOA MBEYA, AZAM KWENDA MORO KOMBE LA SHIRIKISHO

Shirikisho la Mpira wa miguu TanzaniaTFF kwa kushirikiana na wadhamini wa michuano ya kombe la shirikisho Tanzania leo wameendesha droo ya Roundi ya Tatu ya kombe la Azam Sport Federetion Cup ambapo vilabu vya Azam FC na Yanga SC watasafiri kwenda mikoani kumenyana na timu za Ihefu FC na Shupavu FC katika hatua ya 32 Bora ya michuano hiyo

Yanga SC watakwenda Mbeya kuifuata Ihefu, mechi itakayopigwa Uwanja wa Sokoine mjini humo, wakati Azam FC watakwenda Uwanja wa CCM Mkamba mkoani Morogoro kumenyana na Shupavu FC.  

Green Warriors iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba SC itaendelea kucheza nyumbani mjini Dar es Salaam itakapowakaribisha Singida United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.


Timu ya kocha Freddy Felix Minziro, KMC itakuwa mwenyeji wa Toto mjini Dar es Salaam, wakati Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili mfululizo za wenyeji, Kariakoo United dhidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC ya Mwanza na Maji Maji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. 


Maji Maji wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, Kiluvia United wataikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.


Mechi nyingine; Pamba SC wataikaribisha Stand United Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. 


Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 


Mechi zinatarajiwa kucheza siku mbili mfululizo, Januari 31 na Februari 1, mwaka huu.


MECHI ZOTE HATUA YA 32 BORA
KMV V Toto Africans 
Maji Maji v Ruvu Shooting
Njombe Mji v Rhino Rangers
Kiluvia Utd v JKT Oljoro
Ndanda Fc v Biashara United
Pamba SC v Stand United
Polisi TZ v Friends Rangers
JKT Tanzania v Polisi Dar
Ihefu FC v Yanga SC
Mwadui FC v Dodoma FC 
Green Warriors v Singida United
Tanzania Prisons v Burkina Faso
Kariakoo United v Mbao FC
Maji Maji Rangers Lindi v Mtibwa Sugar
Kagera Sugar v Buseresere FC 
Shupavu FC v Azam FC


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.