}

DIWANI AUNDA KAMATI YA WATU 15 KUIJENGA BARABARA YA KATA YA SARANGA.


Diwani wa kata ya saranga kupitia cha cha mapinduzi CCM Mh. Haruni Mdoe ameunda kamati ya watu kumi na tano kuhakikisha kero ya barabara katika kata hiyo inamalizika .

Mh.Mdoe aliunda kamati hiyo katika mkutano wake wa kwanza na wananchi tangu achaguliwe kuwa diwani wa kata hiyo ambapo katika mkutano huo ulilenga kuadiliana juu ya kero kubwa inayo wakabili hasa kero ya barabara.

Akizungumza katika mkutano hou Mh. Mdoe alisema serikali  kupitia taasisi ya ujenzi wa barabara za mitaa TALULA inampango wa kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami katika bajeti ya mwaka 2018 /19.

Mh. Mdoe baada ya kubainisha mpango huo wa serikali aliwaambia wananchi hawawezi kusubiri mpaka mwaka huo kutokana na hali ya barabara hiyo kuwa mbaya kupita kiasi jambo lilimpelekea kuwahamasisha wananchi wake kuchangia kabla ya  serikali kutekeleza mpango wake.

Alisema ipo haja ya wao wenyewe kushirikiana kila mmoja ili kuona hali ya barabara hiyo inabadilika na kupitika kwa ulaisi hata pale Talula watakapokuja itakuwa laisi kwao kuimaliza kwa wakati na katika ubora unaotakiwa.

Baadae Mh.Mdoe aliwataka wananchi wote katika kata hiyo kuwachagua watu watakaoingia katika kamati ya ujenzi wa barabara kutoka kimara Mpaka Matosa ambapo yeye atakuwa mweyekiti wa kamati hiyo.

'kutokana na hali ya sasa ya barabara yetu hatutaweza kusubiri mkapa Talula waje kujenga kulingana na bajeti ya mwaka 2018/19 ,ni ukweli kunapitika kwa tabu sana hata hawa wasafirishaji wetu itafika kipindi hawatakubali kupitisha magari yao tena hivyo hatuna namna nyingine zaidi ya sisi wenyewe kuijenga' alisema Mh. Mdoe.

'Tuunde kamati ya watu watakaotoka katika mitaa yetu yote yaani ule wa michungwani, king'ongo,Matangini na hata kwa majirani zetu kule Matosa  ambako barabara hii inaishia ili tuweka mikakati ya kuanza ujenzi kwa kuchangishana wenyewe kwa wenyewe'.Aliongeza

Aidha Wananchi wote waliofika katika mkutano huo walilipokea suala hilo kwa mkono miwili na kumuhakikishia watakuwa tayari kutoa ushirikiano kwani jambo hilo limekuwa kero kubwa sana kwao.

wananchi hao pia wamewataka wadau wengine wkujitokeza ili kuwasaidia kwani jambo hilo linasadifu maendeleo ya nchi nzima na si Saranga peke yake.

'sisi tupo tayari kuijenga barabara yetu, kwa vile tulivyokuwa navyo tutatoa na hata tutakapohitajika katika kufanya kazi pia tutafanya lakini pia tunawaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia ujenzi huu'.walisema wananchi.

Katika mkutano huo wa kwanza kwa diwani Mh. Mdoe pia alisikitishwa na kitendo cha mwenyekiti wa mtaa wa Michungwani kutohudhulia kwa kile kinachodaiwa wameambiwa wasusie mikutano yote ya diwani huyo.



No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.