}

SUALA LA NYOSO SASA KUJADILI NA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF

Beki wa Kagera Sugar FC, Juma Said Nyosso baada  ya kumpiga shabiki wa wapinzani, katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC,  Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekutana na kujadili suala hilo na kuamua  kulipeleka katika Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya hatua za kinidhamu.

Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichofanyika juzi kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Dar es Salaam.


Katika mechi hiyo namba 112 ambayo Kagera Sugar ilifungwa 2-0, Nyoso alikamatwa na Polisi kwa kumpiga shabiki wa Simba baada ya mechi hiyo iliyochezwa Januari 22, 2018 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.