SHIRIKA LA RELI TANZANIA TRL LIMEFANYA MABADILIKO HAYA USAFIRI WA TRENI.
Na. Happy Shirima.
Shirika la reli Tanzania TRL limehamisha huduma zake za usafiri wa treni kwenda Dodoma kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu ya reli na mvua zinazonyesha maeneo ya kati ya stesheni za kilosa na Gulwe Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kaimu mkurugenzi mtendaja wa TRL Focus Sahani amesemakuwa baada ya kutathimini hali ya miundombinu ya maeneo menginie yaliyo salama wameamua kuhamishia huduma za usafiri wa treni kwa mda mkoani Dodoma.
Hata hivyo amesemakuwa ratiba ya usafiri wa treni ya abiria kutoka Dodoma itakuwa siku za jumanne na ijumaa huku treni ya kutoka mpanda mwanza na kigoma ikifanya safari zake siku ya jumapili na alhamisi.
Bw. Sahani ameongeza kuwa wanaendelea na ukarabati kwenye eneo lililoharibika na kuwaomba radhi abiria kwa usumbufu utakaojitokeza kuanzia January 16 mwaka huu na ambao tayari wameshakata tiketi watarudishiwa nauli zao.
No comments