CHIRWA ASHAMBULI WA NA MASHABIKI BAADA YA KIKOSI CHA YANGA KUWASILI DAR LEO
Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kung’olewa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Wachezaji hao walitua bandarini jijini Dar es Salaam na kupokelewa na basi la klabu hiyo ambalo hutumiwa na kikosi kikubwa cha Yanga.
Baada ya kuwasili Mashabiki wa Yanga wameonekana kushindwa kujizuia baada ya kumvurumishia maneno makali mshambuliaji wao, Obrey Chirwa.
Yanga imetolewa baada ya kufungwa penalti 5-4 na URA ya Uganda na Chirwa ndiye aliyekosa mkwaju wa mwisho.
Mashabiki hao walionekana kumlaumu Chirwa kukosa uchungu na Yanga huku wakimueleza kwamba ametanguliza fedha mbele.
Mshambuliaji huyo raia wa Zambia amejiunga na Yanga siku ya ambayo ilitolewa na URA akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa amekaa siku moja tu baada ya kuwasili akitokea kwao Zambia.
Chirwa aliamua kubaki Zambia akishinikizwa kulipwa fedha zake za usajili.
No comments