}

MKURUGENZI OFISI YA TAKWIMU ATOA ANGALIZO KWA WATOA TAKWIMU.

Na. Happy Shirima.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Albina Chuwa amewataka wadau mbalimbali kuzingatia  sheria ya takwimu katika utoaji wa taarifa mbalimbali  za takwimu rasmi.

 Hayo amesema jijini dar es salaam katika semina na waandishi wa habari iliyoandaliwa na ofisi hiyo ambayo imelenga kutoa elimu juu ya matumizi  mazuri ya sheria ya takwimu ambayo ikitumika vizuri itasaidia kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Aidha amewataka  watu watumie Sheria ya takwimu ya mwaka 2015 kwani haijazuia mtu au taasisi yoyote kutoa takwimu na imetoa wigo na kuweka misingi ya njia bora zinazotakiwa kufuatwa na wadau wa takwimu katika mchakato wa uzalishaji wa takwimu rasmi.

Sambamba na hayo Ofisi ya Taifa ya Takwimu imezindua warsha ya upatikanaji wa takwimu Kwa ajili ya kupima na kutathmini utekelezaji wa mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo na viashiria vya malengo ya  maendeleo endelevu.

Akizindua warsha hiyo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Prof.Faustin Kamuzora amesema kuwa malengo hayo yatasaidia kuleta maendeleo ya uchumi na kijamii pamoja na uendelevu wa mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu  Irenius Ruyobya amesema kuwa Kati ya nguzo tatu kuu za malengo ya maendeleo endelevu mazingira ni moja wapo hivyo ni Jambo muhimu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.