}

KICHUYA ,MAKUDE WAIBUA UCHUNGUZI BENCHI LA SIMBA

Kitendo cha Shiza Kichuya na Jonasi Mkude kwenda kukaa jukwaani baada ya kufanyiwa mabadilko kwenye mchezo wa Mapinduzi Cup dhidi ya URA jana Jumatatu Januari 8, 2018, kimezua mijadala mbalimbali miongoni mwa wadau wa soka wengi wakidai kutakuwa kuna jambo ambalo linaendelea ndani ya timu.
Baadhi ya wadau wanasema kwamba, kitendo hicho kinaashiria kwamba hakuna maelewano kwa baadhi ya wachezaji pamoja na kocha.
Mwenyekiti  wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zacharia Hans Poppe amekiri kwamba kitendo hicho kinaashiria kwamba kuna tatizo la kinidhamu na kuahidi kitashughulikiwa.
“Sijui tatizo ni kitu gani lakini kama kuna sintofahamu zinatokea mpaka mchezaji anatoka anakwenda kwa watazamaji badala ya kwenda kwenye benchi basi pana tatizo fulani la kinidhamu”-Poppe.
“Mchezaji akifanyiwa mabadiliko halafu asirudi kwenye benchi badala yake akaenda kwa watazamaji ni ishara ya protest (mgomo) inaonesha kama hakuridhika na maamuzi ya mwalimu, ni kitu ambacho kitashughulikiwa kujua tatizo ni nini kwa sababu si kitu cha kawaida.”
Kuhusu Simba kutupwa nje ya Mapinduzi Cup mapema, Hans Poppe amesema: “Ni mashindano ambayo tumeshinda mara kadhaa na kuchukua kombe, inasikitisha kama tumeshindwa kufanya hivyo sasa wakati tuna timu nzuri kuliko katika vipindi hivyo ambavyo tulikuwa tukichukua hayo makombe.”

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.