}

YANGA NA MBAO KUUMANA WIKIENDI HII LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA IKIENDELEA

Ligi kuu soka Tanzania bara inatarajiwa kuendelea kuanzia ijumaa wiki hii mpaka jumapili kwa michezo mbalimbali kupigwa katika viwanja tofauti.

katika michezo hiyo Yanga atasafiri hadi huko
Mwanza kuumana na wenyeji wao Mbao Fc ,wakati Kagera Sugar wao wakikipiga dhidi ya Mbeya City. 

Stendi United wao watacheza na Azam Fc huku Mwadui wakiwakaribisha Ruvu Shooting. 

Wekundu wa Msimbazi Simba wao nao watasafiri kuelekea huko Mtwara kuwakabili Ndanda Fc katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, 

Singida United watakuwa wenyeji wa Njombe Mji katika uwanja wa Namfua. 

Mchezo mwangine utawakutanisha Lipuli Fc watakaopapatuana na wajelajela Tanzania Prisons ya kule Mbeya Huku Mtibwa wakiwa Manungu Tulian watawakaribisha Majimaji ya Songea.

Baada ya michezo hiyo ligi hiyo itasimama tena kupisha michuano ya mapinduzi Cup ambayo itapigwa huko Zanzibar  kwa jumla ya wiki mbili.

Vilabu vinne kutoka katika ligi kuuu soka Tanzania bara vitakuwa huko Zanzibar kwa ajili ya michuano hiyo ni Simba Yanga Azam fc Pamoja na Singida United.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.