}

WENYEVITI MSIGANI WATAKIWA KUUNDA VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI

Mkuu wa kituo cha polisi Kimara Kamanda Pius Lutumo amewataka wenyeviti wa mitaa ya kata ya Msigani kuhakikisha wanahamasisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika mitaa yao ili kusaidi kupunguza uhalifu Mitaani.

Akizungumza katika mkutano na wananchi wa kata  ya Msigani ulioandaliwa na diwani wa kata ya hiyo Bw.Mushi Israel Agustino,ukiwa na lengo la kuwataarifu wananchi juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo ya kata na utekelezaji wake kwa mwaka wa 2017.

Kamanda Lutumo alisema kila mtaa unapaswa kuwa na kikundi cha ulinzi shirikishi ili kudhibiti  uhalifu na kujenga amani ya mtaa hivyo ni vyema wenyeviti wa mitaa kuwa mstari wa mbele kuunda vikundi hivyo.

'ukiona mtaa hauna kikundi cha ulinzi shirikishi ujue mtaa huo uko uchi' alisema

'Wenyeviti sasa mnahitajika sana kuhamasisha  katika mtaa kuwa na  vikundi vya ulinzi shirikishi 'alisema kamanda lutumo.

Aidha kamanda Lutumo amesema kazi ya ulinzi ni ngumu hivyo ni vyema kila mtu ashiriki kwa namna moja katika kuhakikisha adhma ya kuwa na amani katika mitaa inakuwepo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Msigani Bw.Mushi Israel Agustino alisema kila mwenyekiti ambaye hataweza kusimamia katika eneo lake la kazi yeye atakuwa wakwanza kuwajibishwa.

Diwani Mushi alisema  wenyeviti wao ndio wako karibu zaidi na wananchi na wanawatambua vizuri waalifu ni lazima wawe wa kwanza kutoa taarifa ili sheria iweze kufuata mkondo wake .

'kama itatokea mwenyekiti analalamika kuwa katika mtaa wake vitendo vya ualifu vimezidi wakati hatoi taarifa za wahusika na vitendo hivyo atawajibishwa kwanza yeye'.alisema diwani Mushi.

Kwa Upande wao mmoja wa walinzi shirkishi alisema kuwa kwa hamasa ambayo leo wamepewa wataenda kufanya kazi kwa juhudi kubwa ili kuhakikisha mitaa yote ya Kata ya Msigani inakuwa na vikundi ambavyo vitafanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa. 








No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.