}

KWASI KIURAINI KUINGIA MSIMBAZI

Uongozi wa klabu ya Lipuli FC umethibitisha kupokea barua kutoka kwa wekundu wa msimbazi Simba inayowataka kuketi mezani ili kufikia muafaka juu ya usajili wa  beki Asante Kwasi.

Akizungumza na kituochahabari.blogspot.com Mwenyekiti wa klabu ya Lipuli Ramadhani Mahano amesema jioni ya leo wanatarajia kukaa na kamati ya utendaji ya klabu hiyo ili kukubaliana juu ya kumuacha mchezaji huyo kwenda kuitumikia klabu ya simba kwa kipindi hiki.

Mahano amesema barua hiyo imewataka uongozi wa klabu hiyo kukua na simba ili kujadili kama kuna gharama ambazo wameziingia kwa mchezaji huyo ili klabu hiyo iweze kuwalipa na kumruhusu Kwasi kuitumikia Simba katika michezo ya ligi kuu na michuano mingine ya kimataifa.

Aidha Mahano ameshindwa kuthibitisha kama wao wako tayari kumuachia mchezaji huyo ingawa benchi la ufundi limewahakikishia usajili walioufanya unaweza kuziba nafasi ya mchezaji huyo pasopokuwa na shida yoyote.

Hata hivyo Mahnoa amewataka wanairinga na mashabiki wote wa soka kukubaliana na maamuzi ambayo yatatolewa na kamati ya utendaji ambayo jioni ya leo inaketi ili kujadili hatma ya mchezaji huyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema wamepeleka barua kwa Lipuli FC baada ya kugundua bado ana mkataba na klabu hiyo pamoja na wakala wake pia.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.