}

WANANCHI KATA YA MZINGA ILALA WAMUANGUSHIA KILIO RAIS MAGUFULI.

Na.Happy Shirima-Dar. 
Wananchi wa mtaa wa magole kata ya mzinga manispaa ya ilala jijini Dar es saalam wamemuomba raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt John pombe magufuli kuwasaidia kutatua kero ya ukosefu wa daraja kwenye mto mzinga ambalo linawasababishia kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo na wanafunzi kushindwa kwenda shule.
Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi hao wamesemakuwa tatizo hilo limekuwa ni la mda mrefu ambapo mvua zinaponyesha mto unafurika na kusababisha kukosekana kwa Mawasiliano baina ya upande mmoja na mwingine huku vijana wakitumia frusa hiyo kuwabeba watu kwa shilingi elfu moja hadi elfu 5.

Kwa upandeke wake mwenyekiti wa serekali ya mtaa wa magole Lucas chacha amesema kuwa, wamekuwa wakitoa taarifa Mara kwa mara kuhusiana utengenezwaji wa daraja hilo bila mafanikio ambapo baada ya kufanyiwa tathimi imeonyesha zinahitajika zaidi ya shilingi bilioni moja ili kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.