}

UPUNGUFU WA MARUBANI NA WAANDISI WAITESA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA.

Na. Happy Shirima-Dar.

Sekta ya usafiri wa anga hapa nchini inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa wataalamu wa usafiri wa anga kwenye maeneo ya marubani na wahandisi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya usafiri wa anga Duniani (ICAD) kaimu mkurugenzi mkuu mamlaka ya usafiri wa anga Vallery Chamlungu amesemakuwa uhaba wa wataalamu unatokana na gharama kubwa ya kuwasomesha ambapo serekali inajitahidi kukabiliana na changamoto hiya.
Aidha ameongeza kuwa sekta ya anga imeweza kupiga hatua kwenye utendaji kazi wake ambapo ukaguzi uliofanywa na mamlaka ya anga kwa nchi wanachama wameweza kufanya vizuri kwa kupata asilimia 65 kutoka 38 walizopata mwaka jana.

Hata hivyo amewataka wananchi kuamini utendaji wa sekta hiyo ambayo imekuwa ukitoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi hasa kupitia sekta ya utalii na wanahakikisha nchi inakuwa na uchumi wa kati na wa viwanda.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.