}

SUMATRA YAWAPA MASHARTI MAPYA WAMILIKI WA MABASI, WAKATAZA BAADHI YA VITU KUFANYIKA NDANI YA BASI.

Na.Anaseli stanley amacha

Baraza la Ushauri la watumiaji wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA CCC limewataka wamiliki wa vyombo vya usafri kufuata masharti ya leseni zao na kutoza nauli ambazo zimeidhinishwa na na sumatra katika kipindi hiki cha sikukuu ya Xmass na Mwaka mpya ambapo watu wengi hurejea makwao ili kuungana na jamaa zao kusheherekea sikuku hizo.

Akizungumza na waandaishi wa habari jijini Dar es salaamu Katibu Mtendaji wa Baraza La Ushauri la Watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini Dkt.Oscar Kikoyo amesema kuna baadhi ya watoa huduma ambao si waaminifu kwa kuchukulia kipindi hiki kama njia ya kuvuna zaidi kutoka kwa watumiaji kinyume cha masharti ya leseni zao.

Dkt. Kikoyo amesema wamaliki wa wa mabasi wanapaswa kuhakikisha wafanyakazi wao wanaokatisha tiketi katika vituo mbalimbali nchini kuwa waaaminifu kwa wateja wao
 
ameongeza kuwa baraza linawataka abiria wanaotarajia kusafiri katika kipindi hiki kufanya maandalizi ya safari zao mapema na kuacha kununua tiketi kutoka kwa wapiga debe  katika maeneo yote ya vituo hapa nchini.

Aidha Dkt. Kikoyo amesema kwamujibu wa kanuni mpya za usafiri za mwaka 2017 haziruhusu kufanya biashara, kuhubiri dini au kuonesha video zisizo na maadili na zisizozingatia utamaduni wa muafrika wakati safari.

katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka watanzania wengi wanasafiri kurudi nyumbani kwao kusheherekea sikukuu za Xmass na mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo utamaduni huo umekuwa kwa kasi na kuchangia kusukuma maendeleo ya vijiji watokavyo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.