}

RAIS MAGUFULI AWATAKA BARAZA NA WANAWAKE KUCHAGUA VIONGOZI BORA

Rais wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Mh. Dkt. John Magufuli amewataka wajumbe wa Baraza Kuu wa Umoja wa Wanawake CCM(UWT) kuchagua viongozi ambao watakuwa wanajali wanawake na siyo kujali mslai yao binafsi.

Akizungumza na wajumbe hao leo Ijumaa wakati akifungua mkutano huo Rais Magufuli amesema watakapokuwa wanachagua viongozi atakae weza kuwa mtetezi na kujali shida za wanawake kwa ujumla  wala mbaguzi. 

“Nataka mchague kiongozi wa kujali wanawake na sio kujali tumbo lake na awe mtetezi na shida zao wala habagui,” amesema Rais Magufuli.

Amesema anawapenda akina mama hivyo wachague mtu kwa matakwa yao.

“Viongozi wa jumuiya hii wanatakiwa kujua historia na kuipigania jumuiya hii muhimu kwa CCM,”

“Wanawake ndio wapigaji kura waaminifu na ukiahidiwa kura nao jua utashinda.”

Amesema, “Chama tunakata kiwe cha wananchi na sio cha mtu binafsi na kiongozi atakayechaguliwa aendane na mabadiliko ya ndani ya chama.”

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.