}

MFANYAKAZI SIMBA CEMENT NA WAWILI WA HALOTEL WATIWA MBALONI KWA WIZI.

Jeshi la polisi mkoani Dodoma linamshikilia mfanyakazi wa kampuni ya saruji ya Simba Cement, Edward Ngassa kwa tuhuma za kutengeneza tukio la uongo la kuporwa Shilingi milioni 20.4 za mwajiri wake.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amesema mbwa wa polisi mwenye mafunzo ndiye aliyegundua udanganyifu huo wa Ngassa nyumbani kwake.
Kamanda Muroto ameongeza kuwa katika tukio lingine wanamshikilia fundi na mfanyakazi wa kampuni ya Halotel Bwa. Ezekiel Muhongole na Bwa. Alfred Mlugu kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa betri mbili za minara ya simu ya halotel katika eneo la changombe na UDOM mkoani Dodoma.
Kamanda Muroto amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na operesheni inayoendelea katika maeneo mbali mbali mkoani Dodoma.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.