}

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE MIRADI YA MAJI.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miradi miwili ya maji katika vijiji viwili vya Rahaleo na Mbungulaji kwenye kata ya Kalulu yenye thamani ya sh. Milioni 112 na kuahidi kumaliza kero ya maji wilayani Tunduru.

Mh Majaliwa  ameyasema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji hivyo ambapo amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Aidha Mh Majaliwa amesema ujenzi wa miradi hiyo ni utekelezaji wa Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani yenye lengo la  kuwafikishia wananchi huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Pia Mh Majaliwa ametoa wito kwa wazee wa vijiji hivyo kwa kushirikiana na vijana kuhakikisha wanalinda mradi huo kwa kutokata miti kwenye maeneo yote yanayozunguka vyanzo vya maji ili kuepusha ukame. Ameagiza ipandwe miti kwenye maeneo hayo ili kuhifadhi mazingira.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.