}

PSPF YAUNGA MKONO JUHUDI ZA DC IKUNGI SINGIDA.

Na Mathias Canal, Singida
Mapema Leo asubuhi Novemba 25, 2017 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekabidhiwa mabati 100 na Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Penseni (PSPF) Mkoani Singida Bi Hafsa Ally kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo.
Mabati hayo yametolewa na PSPF Kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Uongozi katika kuimarisha mfuko wa elimu kwaajili ya kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kuhimiza utatuzi wa Changamoto mbalimbali katika Wilaya ya Ikungi ikiwemo Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.
Akizungumza katika dhifa ya makabidhiano ya mabati hayo iliyofanyika katika eneo la shule ya sekondari Ikungi Mhe Mtaturu ambaye pia ni mlezi wa mfuko wa Elimu amewasihi wananchi na wadau kuchangia fedha au thamani zozote kadri wawezavyo ili kufanikisha kuboresha miundombinu ya elimu katika wilaya hiyo.
Aidha, ameupongeza mfuko huo wa PSPF kwa mpango wao wa uchangiaji wa  hiari ambapo  mwanachama hutakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 , ili kuwa huru kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake ambapo kiwango cha chini kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia kupitia benki.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) Mkoani Singida Bi Hafsa Ally Ameeleza kuwa PSPF ipo karibu na watumishi lakini pia ipo karibu na jamii hivyo wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuwashirikisha kwenye jambo hilo muhimu la kuboresha elimu katika wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla wake.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.