}

WANAHABARI WATAKIWA KURIPOTI MIRADI NA PROGRAMU ZA SADC.

Na.Anaseli Stanley Macha.

 Waratibu wa vyombo vya Habari wa nchi Wanachama  wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)  wametakiwa kuhamasisha vyombo vya habari katika  nchi wanachama kuripoti habari za miradi na progamu zinazotekelezwa na umoja huo kwa manufaa ya wananchi wa nchi wanachama.

Akizungumza katika washa ya ufunguzi Mkuu wa  mawasiliano wa Jumuiya hiyo Bi. Barbara Lopi amesema lengo ni kuwajengea uwezo waratibu hao kuhamasisha vyombo vya habari kutangaza umuhimu wa wananchi kutumia fursa zilizopo katika nchi wanachama kuchochea maendeleo na Ustawi wa umoja huo.

Bi. Lopi ameongeza kuwa warsha hiyo itawajengea uwezo waratibu wa vyombo vya habari wa nchi Wanachama wa namna bora yakushirikiana na vyombo vya habari  katika kutangaza miradi  inayochochea ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama inayotekelezwa na SADC.

Baadhi ya mada zitakazowasilishwa katika warsha hiyo ni pamoja na Muundo wa Jumuiya hiyo,Umuhimu na Majukumu ya Waratibu wa Vyombo vya Habari kwa kila nchi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.