}

WAGOSI WA KAYA WAAMIA KWENYE MAPISHI BAADA YA GEMU YA MUZIKI KUWA TAITI.

Kama ni mfuatiliaji wa muziki nadhani ulishawahi kuwasikia Wagosi wa kaya, ambao walitambulika sana kwa uimbaji wao kwakutumia Rafudhi ya kabila la wasambaa kutokea Mkoani Tanga.

Wagosi wa kaya licha ya kutamba na nyimbo kadhaa ikiwamo Wauguzi na Manesi, kwasasa wamekuwa kimya katika tasnia iyo, kitu kilichopelekea mashabiki wao kuhoji kama bado wanafanya sanaa ama laa.

Hofu ya mashabiki imezidi kutanda baada ya kufuatilia kwa muda mrefu kwenye ukurasa wao wa Instagram nakukosa taarifa yoyote yenye viashiria vya wao kutoa ngoma mpya na badala yake wamejikita kwenye kuelezea na kusifu vitu mbalimbali ikiwamo vyakula vinavyopatikana Rushoto ambako wao wanatokea.

Moja ya posti yao huko Instagram ni hii hapa chini.

#LUSHOTO_KWETU

VIMANDE.

Chakula cha asili ya wasambaa ambacho matayarisho yake ni:

Ndizi za kuiva(uchagani wanatengenezea mbege) kiasi unachotaka kuanzia ndizi 10 ambazo unatoa vimande vipatavyo 4. Au ndizi zaidi ya hapo.

Unazitwanga kwenye kinu huku ukiwa umechanganya na unga wa dona kiasi kulingana na idadi ya ndizi hizo.

Ukishaponda na mchanganyiko ukawa vizuri unachota kiasi na kufunga kwenye jani la mgomba.

Baada ya hapo unachemsha kwenye chungu (kwa huku kwetu) au sufuria (huko nyika/mjini) kwa muda kadhaa ambapo kuiva kwake ukiviminya utaona hali ya ugumu.

Kumbuka hauweki chumvi wala kitu chochote zaidi ya maji kiasi uliyochemshia.

Chakula kitamu sana ukipata na chai ya viungo (iliki,mdalasini) au majani ya mint yale fresh unayoyachuma shamba na asali (kwa huku kwetu) au sukari (huko nyika/mjini)

#Vimande
#NtajaUshe

Nyumbani ni nyumbani.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.