}

SIMBA VS URA JANUARI 2 KOMBE LA MAPINDUZI


SIMBA SC itafungua dimba na URA ya Uganda katika michuano maarufu ya Kombe la Mapinduzi, Januari 2, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan, Zanzibar mchezo ambao utaanza Saa 2:15 usiku.

Mahasimu wao, Yanga wataanza na JKU ya Zanzibar Januari 1, Uwanja wa Amaan pia, mchezo ambao nao utaanza Saa 2:15 usiku.


Mabingwa watetezi, Azam FC wataanza na Jamhuri katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Amaan pia Januari 2, lakini kuanzia Saa 10:15 jioni. 


Ufunguzi rasmi wa Kombe la Mapinduzi 2018 utafanyika Desemba 30, mwaka huu kwa mechi mbili kuchezwa Uwanja wa Amaan, kwanza Zimamoto na Mlandege Saa 10:17 jioni na baadaye JKU na Shaba Saa 2:15 usiku. 
       
 Kundi A 
Simba
Azam FC, 
Jamhuri, 
Taifa ya Jang’ombe na 
URA ya Uganda, 

Kundi B
Yanga 
JKU, 
Mlandege, 
Zimamoto na 
Shaba.

Simba itamenyana na Azam FC Januari 6, ikitoka kukipiga na Taifa ya Jang’ombe Januari 4, kabla ya kumalizia mechi zake za Kundi A Januari 8 na Jamhuri.

Azam FC itacheza na Taifa ya Jang’ombe Januari 4 kuanzia Saa 10:15, kabla ya kumenyana na Simba na itahitimisha mechi zake za Kundi A kwa kuumana na URA Januari 8 Saa 10;15 pia jioni Uwanja wa Amaan.


Baada ya mechi na JKU, Yanga watarudi tena uwanjani Januari 3 kwa mchezo na Shaba, Januari 5 na Zimamoto kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Mlandege Janauri 7 Uwanja wa Amaan.


Nusu Fainali zinatarajiwa kuchezwa Januari 10 na Fainali itakuwa Januari 13, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan kuanzia Saa 2:15 usiku.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.