}

MTIBWA YAREJEA NA KUENDELEA NA MAZOEZI MANUNGU

BAADA ya ushindi wa mechi mbili mfululizo za kirafiki mkoani Lindi, Mtibwa Sugar inarejea Turiani mkoani Morogoro kuanza maandalizi ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Afisa habari wa klaby ya Mtibwa  Thobius Kifaru amesema kwamba kikosi   leo mchana kimewasili  Turiani kwa basi lao walilopewa hivi karibuni na wamiliki, Superdoll. ambapo kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya michezo mingine ya ligi kuu Tanzania bara

Kifaru amesema pamoja na kasi yao kupungua bado wanaamini kuwa watarejea kileleni hivi karibuni

KATIKA MECHI IJAYO Mtibwa watakuwa wenyeji wa ndugu zao, Kagera Sugar ya Bukoba katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Novemba 18, Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.