}

KAMPUNI SITA ZA MAWASILIANO ZAPIGWA FAINI YA SHILINGI BILIONI 11

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitoza faini ya Sh bilioni 11 kampuni sita za simu kwa kutofuata taratibu za usajili wa laini za simu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema, kampuni  hizo zimepigwa faini kutokana na kusajili laini mpya bila kutumia vitambulisho vinavyotakiwa.

Aidha Bw.Kilaba amezitaja Kampuni hizo  ambazo zimepigwa faini kuwa Halotel ambayo imetozwa Faini Sh bilioni 1.6, kampuni ya Smart Sh bilioni 1.3, Airtel Sh bilioni 1.08, Vodacom Sh milioni 945 na Zantel Sh milioni 105.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.