}

CHAMA; SASII AMEFANIKIWA KUTAFSIRI SHERIA 17 KATIKA MECHI YA YANGA NA SIMBA

Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Tanzania Salumu Umande Chama amesema mwamuzi Heri Sasii amefanikiwa kwa asilimia kubwa sana kataika kutafsiri sheria 17 za mchezo wa soka katika mechi ya watani wa jadi Yanga N simba Mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1  1.

 katika malalamiko ambayo wekundu wa msimbazi simba wana yalalamikia hasa ya kunyimwa penalti  Chama amesema si kila mpira unaogonga mkono unaweza kuwa penalti hivyo ni vyema wakasubiri kamati ya saa 72 ichunguze na kutoa maamuzi.

Aidha Chama amesema  mpaka sasa bado hawajapokea barua yeyote kutoka kwa klabu ya simba ambayo imeonesha malalamiko juu ya waamuzi katika michezo ya na pale watakapoipata wataifanyia kazi mapema. 




No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.