}

VITUO VYA POLISI NA MAGEREZA KUONGEZWA RASMI NCHINI.

Na. Anaseli Stanley Macha.

Naibu Waziri wa mambo ya Ndani Mh. Hamad Masauni akichangia jambo Bungeni mjini Dodoma. 

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Hamad Masauni amesema serikali inampango wa kujenga vituo vya polisi katika wilaya 65 na magereza katika wilaya 52 nchini.

Mh masauni amesema hayo wakati akijibu swali la Mh. Shukuru Kawambwa mbunge wa bagamoyo aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kujenga nyumba za polisi na askali magereza bagamoyo ikiwemo ukarabati wa kituo cha polisi na Gereza la kigongoni bagamoyo.

Mh. Masauni amesema serikali inampango wa kukarabati vituo vya polisi na magereza pamoja na kujenga vituo vya polisi,nyumba na magereza katika eneo la bagamoyo kwa awamu kulingana na mfuko wa bajeti.

Kwaupande wake waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba amesema mgogoro kati ya gereza la kigongoni na wananchi utapatiwa ufumbuzi na wilaya zote za ukanda wa mkuranga zitapewa kipaumbele kwa kujenga myumba za polisi,ofisi na askali wengi ili kuakikisha usalama wa wananchi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.