}

YANGA YAMPA KITENGO MKWASA

Uongozi wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara,timu ya soka ya Yanga leo hii umemtamburisha aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charse Boniphace Mkwasa kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clementi Sanga amesema kwamba uongozi umeamua kumpa majukumu Mkwasa kutokana na uzoefu wake alio nao katika sekta ya michezo hivyo anaamini mchango wake utakuwa na tija kubwa katika klabu hiyo.

Sanga amesema kwamba awali nafasi hiyo imekuwa ikishikiliwa na Baraka Deusdedit aliyekuwa anakaimu,lakini kwa sasa uongozi umempa majuku ya kuwa mkurugenzi wa fedha ili kuendelea na majukumu hayo kwa lengo la kuboresha mipango ya timu.


Kwa upande wake Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba anaamini nafasi hiyo ambayo ameipata ataitendea haki kwani ana uzoefu mkubwa wa kwenye sekta ya mpira wa miguu hivyo ni vyema mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kutokuwa na hofu juu yake hasa katika utendaji wa kazi.

 Katika hatua nyingine Mkwasa amesema kwamba katika utendaji wake wa kazi hatoingilia majukumu mengine ambayo hayamuhusu ikiwemo kwenye benchi la ufundi lakini pindi msada wake utakapohitajika hatosita kusaidia kwa kile anachoona kitakuwa na tija kwa klabu.
 

Nae aliyekuwa anakaimu nafasi ya katibu mkuu wa klabu hiyo,Baraka Deusidedit amewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kumpa ushirikiano wa kutosha katibu mkuu mpya Charse Boniphace Mkwasa kama walivyofanya wakati wa uongozi wake.
 
Baraka amesema kwamba,Mkwasa ni miongoni mwa watu ambao wanaoufahamu vizuri mpira wa miguu hivyo kuwepo kwake ni faida kubwa kwa klabu kwenye maendeleo ya mpira wa miguu.




No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.