}

AZAM KUKIPIGA NA MABIGWA AFRIKA KESHO SAA MOJA USIKU

uongozi wa klabu ya Azam ya jijini Dar es salaam umesema kwamba kikosi chao hapo kesho kunako mishale ya saa moja usiku kinataraji kushuka dimbani kucheza na mabingwa wa klabu bingwa barani Afrika Mamelod Sundowns

Afisa Habari wa Azam FC,Jafary Idd amesema kwamba ingawa awali hawakuwemo kwenye mipango ya kucheza mchezo huo sambamba na kutomfahamu mratibu wa mchezo huo kwa upande wao wameamua kucheza kwa ajili ya kulinda ushirikiano kwa nchi husika pamoja na klabu.

Amesema kwamba wanacheza mchezo huo huku wakibanwa na ratiba ya ligi kuu ya Tanzania bara kwani siku ya jumamosi watacheza mchezo wa ligi lakini kwa kutambua mpango huo wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya kudumisha umoja wao.

Jafary amesema kwamba katika mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watawakosa huduma za wachezaji wao wawili muhimu John Boko pamoja na Stephen Kingue ambao hawa wote ni majeruhi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.