}

WANA MWANZA KUUJENGA UWANJA WA CCM KIRUMBA


Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba Ndg Steven E. Shija amepokea Mifuko 35 ya Saruji yenye thamani ya Tshs 527,000/= kutoka kwa wajasiliamali na Mafundi wa eneo la Uwanja, mifuko hiyo imeongeza idadi kufika 60 bado mifuko 40 ya Saruji.

Mifuko hiyo imekabidhiwa na Ndg Michael Omolo ambaye ni Mwenyekiti wao, amekabidhi mbele ya Wajasiliamali na Mafundi wote pia ameahidi kupitia umoja wao wataendelea kusaidia ujenzi wa Mkondo wa maji uliopo nje ya Uwanja maana kutokuwepo kwake kunaathiri shughuri zao wakati wa Masika, Hivyo kuleta athari kwenye kipato Chao.

Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba, aliwashukuru sana Watu wote waliojitolea kuchangia ndani ya umoja huo wa Mafundi na Wajasiliamali katika maeneo ya kiwanja, aliwahidi kuendelea kuwapa ushirikiano na kuimarisha mahusiano aliyoyaanzisha maana anaamini hakuna jambo jema na endelevu linaweza kufanywa na yeye peke yake bila kushirikiana nao pamoja na wadau wengine wenye nia njema na endelevu.

Pia aliwashukuru kwa utayari wao wa kuendelea kusaidia ujenzi wa kurejesha mfumo wa Mkondo wa maji nje ya Uwanja wetu, zaidi aliwasihi kuwa wanaowajibu wa kuhakikisha mazingira ya Kazi zao yanakuwa masafi kila wakati pamoja na kuitumia vyema Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi kushirikiana kufanya Usafi kwa maeneo yao ya Kazi.

Mwisho, Meneja wa Uwanja aliendelea kuwaomba wadau mbalimbali kuendelea kusaidia kuchangia juhudi hizi ili kazi hii ifanyike mapema sana, kwa maana kazi hii siyo nyepesi.

"We walk the Talk "

Imetolewa na:-
Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba - Mwanza

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.