}

MANARA AWAITA MAPOYOYO WANAOTAKA SIMBA KUPOKWA POINT

Baada ya kuwepo kwa taarifa juu ya simba huenda ikapokwa alama tatu zilizotokana mchezo wao dhidi ya Polisi Dar kwa kumuweka benchi mchezaji Lufunga ambaye katika michano hiyo hiyo mwaka jana mchezaji huyo alikuw kadi nyekundu jambo ambalo limeadiwa kuwa hakustahili kucheza au kukaa benchi katika mchezo huo.

Leo afisa habari klabu ya simba Haji S Manara ametoa wataka washabiki wa klabu hiyo kuwapuuzia watu hao .

Na haya in maneno take Manara...

kuna vitu vikitokea, kwa mtu mwerevu hutakiwa kunyamaza kimya, hususan kama vitu vyenyewe ni vya hovyo hovyo,
hasa vikitoka kwa watu mapoyoyo wasiojitambua.

 lakini kuna vingine kwa faida yenu wanasimba wenzangu, ni wajibu wangu kuyajibu hata kama limezushwa na mapoyoyo.

Ktk siku za karibuni mapoyoyo wamekuwa na utaratibu wa hovyo hovyo kutumia mitandao ya kijamii kufanya propaganda chafu au niziite nyeusi za kutunga uzushi wa kila aina juu ya klabu yetu, na wakati mwingine huzusha hata yasiowahusu.

kiasili poyoyo ni binamu yake pwagu na huwa ni swahiba mkubwa na pwaguzi, hawa wote siku hzi wameamua kucheza na mitandao ili watutoe njiani.

Wote mwakumbuka ule uzushi juu ya vibali vya wachezaji wetu wa nje, na zile ngonjera zao za Simba kupokwa points za mechi ya Ndanda, najua mwakumbuka zile hekaya zao juu ya wachezaji wetu Ajibu na Tshabalala, kilichotokea nyote mwakijua.

 Mapoyoyo juzi wakazusha la Mkude na kulisambaza kwa kasi mitandaoni, Tukalipangua kama twala sufi.

Mapoyoyo jana wakauzua hili la Lufunga!!
niwaambie mpira unachezwa na kanuni na sheria, hauchezwi mitandaoni na vinywani, wasitutoe ktk umakini wetu na mchezo dhidi ya Azam, Simba ni klabu kubwa mno, hao mapoyoyo zao ni propaganda, zao ni hekaya, zao ni porojo na ufukunyuku tu.

waache blah blah, waweke mziki, eti tutanyang'anywa ushindi dhidi ya Police, na maskini ya Mungu maafande nao wamewasikiliza mapoyoyo wa mtandaoni, eti wamekata rufani, hihihihihi,

Tuwaache mapoyoyo wazushe, cc tufocus na lamba lamba jumamosi, puuzeni mapoyoyo, puuzeni *black propaganda* za kina chakubanga na Poyoyo.

*HAJI S MANARA*

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.