}

Wizara ya mambo ya nje ushirikiano wa kimataifa imepokea msaada wa milioni 180


Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki imepokea msaada wa shilingi milioni 108 kutoka jamhuri ya korea kwaajili ya kuwasaisia wahanga pamoja na ukarabati wa miundombinu iliyoharibika na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Akipokea masaada huo Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Dkt.Augustino Mahiga amesema serikali ya korea imekuwa ikichangia masuala mbalimbali ya kiuchumi na utoaji wa misaada ya kibinadamu hivyo mchango huo ni ishara ya mahusiano mazuri yaliyopo baini ya Tanzania na Korea.

Balozi Dkt. Mahiga ameongeza kuwa msaada huo utaunganishwa na misaada mingine iliyopokelewa awali na kuishukuru jamhuri ya Korea kwa msaada huo.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Korea Song Geum Young amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuimarisha mahusiano huku tanzania ikitarajia kuanzisha ubalozi mjini Seoul.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.