}

Korea Kaskazini Wadukua taarifa za Jeshi la Korea Kusini.


Wataalamu wa mawasiliano ya Internet wa Jeshi la Korea Kusini, wajipanga kuimarisha ulinzi zaidi dhidi ya watu wanaodukua taarifa zao (Hackers) hasa Korea Kaskazini.

Msemaji wa Jeshi la Korea Kusini amesema wamegundua kuwa kuna baadhi ya taarifa zao zinaibiwa ingawa hawajaweka wazi ni taarifa gani hasa zinazodukuliwa.

Korea Kaskazini imewahi kutuhumiwa kudukua taarifa za ma Bank na vyombo vya habari, lakini haikuwah kutuhumiwa juu ya udukuzi wa taarifa za majeshj ya Korea Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa za mtaalamu wa kompyuta wa Korea kaskazini Profesa Kim Heung Kwang, Korea kaskazini inaaminika kuwa na Maelfu ya wataalamu wa kudukua taarifa kwakuwa tangu mwaka 2010wamejikita katika utengenezaji wa programs za kompyuta unaoweza kuvamia na kuharibu miundombinu ya Mawasiliano ya Taifa.

Mpaka Juni mwaka huu kompyuta zaidi ya Laki moja na Elfu arobaini (140000) za makampuni 160 yamevamiwa nakudukuliwa taarifa zake na Korea kaskazini, kwamujibu wa Polisi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.