}

Wataalam waichunguza ajali ya Ndege ya Chapecoense.


Baada ya ajali ya Ndege ya chapecoense kutokea Jana nchini colombia, tayari timu ya wachunguzi wa ajali za anga wa Uingereza Ipo nchini humo kusaidia kujua kwanini ndege hiyo ilianguka.

Mtaalamu wa zamani wa uchunguzi wa tawi la uchunguzi la ajali za anga (AAIB) Stephen Moss ambaye amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 35 amesema, wataalamu hao wamegawanyika katika makundi matatu
1.Wataalamu wakuchunguza mwenendo wa Rubani alivyokuwa akirusha ndege.
2. Waandisi wa Ndege
3.Wataalamu wanaodili na kifaa maalumu chakurekodi nakutunza kumbukumbu katika Ndege (Black box) .

Moss amesema watatakiwa kuchimba nakutafuta kifaa hicho kwauangalifu mkubwa, nakutokitegemea sana katika uchunguzi wao kwakuwa hakiwezi kutoa kila taarifa watakayo hasa kinapokuwa kimelowa nakutokaushwa kitaalamu katika kabati lakuchomea (Heated Cabinet).

Pia nilazima waainishe namna ambavyo ndege ilianguka, kwakupiga ardhini au kwa namna yakutaka kutua.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.