NYUMBA ZA MADANGURO UWANJA WA FISI KUBOMOLEWA.
Dar mpya inawezekana ikiwa kila mmoja wetu na kwa pamoja tuta shikamana kwa kufanya Kazi kwa bidii kila mtu katika nafasi yake ,lakini sikwa ulevi wala wala kuendesha biashara haramu.
Nibaadhi ya maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh Paul makonda , aliyo yasena wakati alipo tembelea uwanja wa fisi tandale ambapo alikutana na baadhi ya nyumba zina endesha biasha ya madanguro akiwa ame ambatana na Mkuu wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Kamishina Simon Sirro,na RPC wa Kinondon Suzana kaganda na waandishi wa habari.
Makonda alilazimika kugonga mlango katika moja ya nyumba zinazo sadikiwa kuwa ni ni danguro lakini watu walio kuwemo humo waligoma kufungua mlango .
Katika eneo hilo pia kulikuwa na watu wakinnywa pombe za kienyeji ambapo hali ya watu hao ili kuwa mbaya akalazimika kuuliza maswali ya kuwapima ufahamu "we we Rais wa Tanzania ninani? majibu ni Nyerere ,ni ....mimi.
No comments