ARSENAL YAFANYA USAJILI WA KUVUNJA REKODI YA DUNIA , LIVERPOOL IKIVUTA MKWANJA MREFU
Klabu ya soka ya Arsenal ya wanawake wamefanya
usajili wa rekodi ya dunia kwa kumsajili mshambuliaji Raia wa Canada Olivia
Smith kutoka klabu ya Liverpool kwa kitita cha Euro million 1.
Olivia Smith anakuwa mchezaji wa kwanza kwa wanawake
kufikia rekodi kusajiliwa kwa gaharama kubwa duniani
Smith mwenye umri wa miaka 20 akiwa na klabu ya Liverpool
amecheza michezo 20 ya ligi kuu ya wanawake England na kufunga magoli saba.
Uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Arsenal unavunja
rekodi ya mchezaji Naomi Girma aliyesajiliwa na Chelsea mwezi januari kwa
kitita cha Euro laki 9.
No comments