SACP. NYAMKA ASISITIZA NIDHAMU KWA ASKARI.
Na. Geofrey Jacka - Dodoma
Kaimu Kamishna wa huduma za Urekebu Jeshi la Magereza, SACP. Ramadhan Nyamka, leo Oktoba 29, 2021 ameongoza Baraza la Maafisa, Askari na watumishi Raia wa Makao makuu ya Magereza.
Baraza hilo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida kila mwisho wa mwezi hufanyika, ili kujadili mambo mbalimbali ambapo Wajumbe hupata fursa ya kuchangia Ajenda zinazowekwa mezeni.
Katika Baraza hilo Wajumbe wamesisitizwa juu ya umuhimu wa kujiwekea akiba huku suala la kuimarisha mfuko wa maafa likiwekewa mkazo ili kuhakikisha mfuko huo unaendelea kufanyakazi, kwani umekuwa na msaada mkubwa hasa wakati wa Matatizo.
Akizungumza kabla ya kufunga baraza hilo SACP. Nyamka pamoja na ajenda nyingine amesisitizia suala la Nidhamu kwa Maafisa na Askari kwani ndio msingi mkubwa katika kazi.
No comments