}
­

MKUTANO MKUU TPS SACCOS KUANZA NOVEMBA 18, 2021 JIJINI DODOMA.

 Na. Geofrey Jacka-Dodoma


Katika kujiandaa na Mkutano Mkuu wa TPS SACCOS utakaoanza kesho Novemba 18, 2021, katika ukumbi wa Meja Gen Mzee, Msalato Jijini Dodoma, Wajumbe wa Mkutano huo wamekutana leo kwaajili ya kupatiwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo, ili kuwa na ufanisi katika kujadili Ajenda za Mkutano huo.

Akizungumza katika Semina hiyo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa Mkutano huo, mtoa mada ambaye ni mtaalamu wa masuala ya vyama vya Ushirika Dkt. Uronu amesema kuwa, wajumbe na wanachama wa TPS SACCOS wanapaswa kushikamana na kujua malengo ya Chama hicho, ikiwa ni pamoja na kusoma kanuni zinazoongoza vyama vya Ushirika, ili kuifanya Sacco's hiyo kusonga mbele.


Aidha wawakilishi wa Mkutano huo wamepata nafasi ya kuchangia hoja mbalimbali ikiwemo kiasi cha uchangiaji, huku wakiutaka uongozi wa ngazi za juu wa TPS SACCOS kupita katika vituo nchi nzima, kwa lengo la kutoa elimu kwa wanachama, kitu walichodai kitakuwa msaada, kwani ufafanuzi utakao tolewa na viongozi hao utakuwa ni wa kina, ukilinganisha na ule unaotolewa na wawakilishi wanaopatikana katika vituo husika.



Mkutano huo unatarajiwa kuwa wa siku mbili, ambapo utaanza Novemba 18, na kumalizika Ijumaa Novemba 19, huku wajumbe na wageni waalikwaa kutoka katika Sacco's nyingine wanatarajiwa kufikia 274, ambapo Mgeni rasmi atakayefungua mkutano huo ni Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Christopher .D. Kadio.


Kwa habari zaidi kuhusu Mkutano huu, endelea kuwa nasi katika Blog hii.


PICHA ZAIDI👇🏻







Kwa maoni na ushari, wasiliana na Mwandishi.

Email. geofreyjacka308@gmail.com 
0659794337 / 0625972465

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.