}

Tanzania kushiriki mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje nchini Ethiopia.

Na. Anaseli Stanley Macha.


Tanzania inatarajia kushiriki mkutano wa nne wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za afrika na korea ambao utafanyika kwa mara ya kwaza barani afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia desemba 6 hadi 7 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijni Dar es salaam msemaji wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki Mindi Kasiga amesema lengo la mkutano huo ni kukuza ushirikiano na kuandaa maeneo mapya ya ushirikaano baina ya korea na mataifa ya afrika kwa miaka 3 ijayo.

Bwa. Kasiga amesema kuwa Tanzania ni moja kati  ya nchi nne za afrika ambazo korea imezichagua kuanzisha mahusiano ya kimikakati itakayo ziwezesha nchi hizo kupewa kupaumbele cha kupokea mikopo nafuu na misaada kwa kipindi cha miaka 5.

Ameongeza kuwa katika kipindi hicho Tanzania itapokea kiasi cha dola za kimarekani milioni 300 ambazo ni sawa na asilimia 17.1 ya msaada utakao tolewa barani afrika.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.