}

Januari Makamba: Tuinusuru nchi kuwa jangwa.

Na. Anaseli Stanley Macha. 


Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mh. Januari Makamba amefanya mazungumzo na wahariri na waandishi wanaojihusisha na masuala ya hali ya mazingira nchini na kueleza kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kuchukuliwa ili kunusuru nchi kuwa jangwa .

Akizungumza katika mkutano huo Mh. Makamba amesema amefanya ziara ya siku 16 katika mikoa 10 kujionea hali ya mazingira na uharibifu Mkubwa wa vyanzo vya maji ikiwemo uharibifu mkubwa katika ziwa Rukwa ambalo kina chake kinapungua kutoka mita 9 hadi 6.

Mh. Makamba amewataka wanahabari kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi wa mazingira ikiwemo kupanda miti,kuitunza,kutotupa ovyo taka ngumu za plastiki,kutolima katika vyanzo vya maji na kutotumia sumu wakati wa kuvua samaki.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.