}

Rais wa Simba Evans Aveva aitisha kikao Jumamosi ijayo.

Na. Anaseli Stanley Macha.
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva. 


Rais wa klabu ya Simba Bwana Evans Aveva atakuwa na Mkutano na viongozi wa matawi ya klabu ya Simba siku ya Jmosi ya tarehe 3-12-2016 saa Nane mchana,kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu,uliopo barabara ya Msimbazi, jijini Dar es salaam. 

Mkutano huo ni maandalizi ya Mkutano mkuu maalum wa tarehe 11-12-2016 ambao utafanyika kwenye bwalo la maafisa wa Polisi Oysterbay jijini hump. 

Pamoja na hayo,mkutano wa Rais na viongozi wa matawi,utajadili kwa kina maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini, inayotarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu.

Katika taarifa yake msemaji wa Simba bw.Manara, amewataka  viongozi wote wa matawi kujitokeza bila ya kukosa katika mkutano huo ambao ni muhimu sana kwa mustakbali wa Klabu ya Simba.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.