}

Mfahamu msichana wa miaka 9 anayeisumbua Dunia katika mchezo wa Ngumi.

Tajamul Islam, ni mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa kutoka India, ambaye ameshinda mataji mengi ya mchezo wa Ngumi, la mwisho ikiwa ni Novemba mwaka huu huko Italy.

Tajamul anatokea katika kijiji cha Bandipora umbali wa Kilomita 65 saw a na mail 40 kutoka mji mkuu wa Srinagar huku akiwa ni mtoto wa familia yenye maisha ya kawaida ambapo baba yake anafanya ni Dereva katika kampuni ya ujenzi na analipwa kiasi cha Rupee 10000 sawa na Dolla 146 kwa mwezi.

Alianza mchezo wa ngumi akiwa mdogo zaidi na amewahi kushinda medali ya Dhahabu katika mji wa Jammu mwaka 2015 na nyingine aliipata katika mashindano ya mchezo wa ngumi wa kitaifa nchini India mwaka huohuo 2015 akiwashinda wapiganaji wengine waliomzidi umri.

Tajamul alijiunga na kituo cha ndani cha kufundisha ngumi (Local Martial Arts Training Academy), nakila siku hufanya mazoezi makali ikiwemo kupiga ngumi nyingi katika gunia la mchanga,  na inakadiriwa hufanya mazoezi kwa zaidi ya masaa 25 kwa wiki, chini ya mwalimu wake Faisal Ali.


Mapema mwezi huh Tajamul ameshinda medal ya Dhahabu katika mashindano ya Dunia ya Ubingwa wa mchezo huo kwa watoto ambapo Mataifa 90 yalishiriki na alifanikiwa kuwashinda wapinzani wake kutoka China, Japan, Ufaransa, Italy, Canada na Marekani.

Tajamul amekuwa maarufu na mfano wakuigwa huku akiweka wazi ndoto sake zakuwa Daktari Ili atakapopigana nakuwavunja wapinzani wake aweze kuwatibu mwenyewe.



No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.