}

Mbeya City , Ndanda FC wajifua vikali kuwakabili Wapinzani wao.


Kikosi cha timu ya soka ya Mbeya City,kwa sasa kinajiandaa vyema kwa ajili ya pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Toto Afrika ya jijini Mwanza,mechi inayotaraji kupigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Msemaji wa wagonga nyundo wa Mbeya City,Dismas Ten,amesema kwamba kwa sasa nia yao ni kuona wanapata pointi tatu muhimu,baada ya kushindwa kupata pointi hizo katika mchezo wao uliopita mbele ya Kagera Sugar.
Amesema kwamba pia amepata taarifa kutoka kwa daktari wa timu hiyo ambapo kuelekea kwenye mechi hiyo wanataraji kukosa huduma za mlinzi Haruna Shamte baada ya kupata maumizi kwenye mchezo wao uliopita.
Aidha amedai kuwa mchezaji wao Mrisho Khalifan Ngasa aliyesajiliwa katika dirisha dogo la mwezi november anataraji kuwemo kwenye mechi hiyo ya jumamosi,baada ya kuwepo kwa dalili za kupatikana kwa ITC yake kutoka Omani.

NDANDA FC


Uongozi wa timu ya soka ya Ndanda ya mkoani Mtwara,umesema kwamba kikosi chao kimejiandaa vyema kuwakabili Mtibwa Sugar katika pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara linalotaraji kupigwa siku ya jumamosi mkoani humo.
Msemaji wa timu hiyo,Idirsa Bandali amesema kwamba kwa upande wao kila kitu kipo vizuri kuelekea kwenye mchezo huo na wanataraji kuingia na tahadhari kubwa hasa baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye mechi iliyopita mbele ya Simba.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.