}

Jeshi la Polisi latoa tahadhari hii msimu huu wa sikukuu.

Dar es salaam - Tanzania. 


Katika kuelekea sikukuu ya xmass na mwaka mpya  ambapo wananchi wenye imani ya kikristo  na hata madhehebu mengine hutumia huo mda kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mengine ya starehe . Uzoefu unaonesha kwamba sikukuu hizi za mwisho wa mwaka huambatana na vitendo vinavyohatarisha usalama wa raia na mali zao ambapo baadhi ya watu kutumia vlevi kupita kiasi, kujipatia kipato kwa njia ya udanganyifu ,wizi ,unyang'anyi pamoja na uendeshaji wa vyombo vya moto bila kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani .

Kufuatia matishio hayo , Jeshi la polisi nchini limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba wanasheherkea sikukuu hizo kwa amani na utulivu bila kuwepo kwa vitendo vyovyote vya uhalifu .Ulinzi umeimarisha kwenye maeneo yote ya kuabudia ,fukwe za bahari ,na sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mkusanyiko mikubwa ya watu


Aidha jeshi la polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa kutoa taarifa kupitia namba za makamanda wa polisi wa mkoaa na na mba za bure 111 na 112 pindi wanapoona viashiria  vyovyote vya uhalifu katika maeneo mbalimbali na watokapo kwenye makazi yao wasiache nyumba wazi ama bila mtu na badala yake watoe taarifa kwa majilani zao.pia jeshi la polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabrani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini


Wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezpo wa kumbi hizo badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi .Vilevili wazazi wawe makini na watoto wao ili kuepuka upotevu wa watoto ,ajali na matukio mengine yanaweza kusababisha madhara juu yao. Hali kadharika wamiliki wa maduka makubwa tunawakumbusha kufunga kamera za CCTV ili kurekodi mienendo ya watu wanaoingia na kutoka katika maduka yao kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali na kuweza kubaini uhalifu na wahalifu kwa haraka 


mwisho napenda kuwahakikishia wananchi kwamba jeshi la polisi linatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria za nchi hivyo halitawajibika kumuonea huruma ama upendeleo kwa mtu yeyote atakaeenda kinyume na sheria .


IMETOLEWA NA.
Kamishina msaidizi wa polisi (ACP) Advera John Bulimba,
Msemaji wa jeshi la polisi
makao makuu ya polisi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.