}

Uhuru Suleiman Alikandia soka la Bongo, asema linautofauti na nchi nyingine.


Mtanzania anaecheza soka nchini Afrika ya Kusini,Uhuru Suleimani,amesema kwamba kuna utofauti mkubwa sana kwa mtu anaecheza hapa nyumbani na yule anaecheza soka la kulipwa katika nchi nyingine.
 
Uhuru Suleimani amesema kwamba utofauti uliopo ni pamoja na ushindani kwa wachezaji pamoja na maslahi ya mchezaji husika,huku pia mchezaji anapofanya vizuri ana asilimia kubwa ya kupata ofa ya kusajiliwa na timu nyingine kwani mawakala wengi huwa wanafuatilia wachezaji kwenye ligi zenye ushindani. 
 
Katika hatua nyingine Uhuru,amesema kwamba ukosefu wa wadhamini kwa baadhi ya timu za Tanzania ambazo zinashiriki ligi kuu ndio chanzo cha ligi hiyo kutawaliwa na vilabu vitatu vya Simba,Yanga na Azam.
 
Amesema kwamba vilabu vingi vya Tanzania havina udhamini hivyo ni kazi kubwa kwa timu hizo kushindanana na timu tatu za Simba,Yanga na Azam kwakuwa hazina uwezo wa kujiendesha kwa weledi ikiwemo kulipa mishahara inayokidhi matakwa ya mchezaji..

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.