}

Farid Mussa wa Azam Fc Atimkia Hispania kuichezea Derpotivo Tenerif


Baadaya ya kuzuguka kwa muda mrefu kutafuta vibali vya kuweza kucheza soka nje ya nchi mchezaji wa klabu bingwa afrika masahariki na kati Azam Fc, Farid Mussa, sasa  amekamilisha taratibu zote ambazo zilimuhitaji kuzifuata na hapo kesho anatarajiwa kuanza safari yake ya kwenda nchin hispania kuitumikia klabu ya Deportivo Tenerif ya chini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari afisa habari wa klabu hiyo Jafari Idd Maganga amesema faridi ataondoka hapo kesho kwa ndege ya KLM, katika mjira ya saa tano usiku baada ya taratibu za kuondoka kwake kuwa zimekamilika na timu ya Tenerif tayari imetuma tiketi  yake.

Aidha  maganga ameeleza kwamba klabu imemtakia kila la heri mchezaji huyo na kumtaka acheze kwa mafanikio makubwa jambo ambalo litafungua milango kwa wachezaji wengine kupata nafasi za  kucheza soka la kimataifa.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.