}

ACT wazalendo ya Zitto Kabwe, yatoa neno Uchaguzi Zanzibar


Afisa Habari wa Chama cha ACT Wazalendo Bw. Abdallah Khamis ametoa taarifa rasmi juu ya tarehe ya kuanza kampeni katika jimbo la Dimani Visiwani Zanzibar.
taarifa hiyo imeeleza kuwa kampeni  kwa ajili ya chama cha ACT Wazalendo katika jimbo la Dimani visiwani Zanzibar na kata mbali mbali kwa Tanzania bara ambazo chama kimesimamisha wagombea zitafunguliwa rasmi disemba 31/2016”
Taarifa imeongeza kuwa, chama kilisimamisha wagombea saba na waliopitishwa na Tume ya uchaguzi ni wagombea sita baada ya mgombea wa Kata ya Misugusugu mkoani Pwani kuenguliwa kugombea kutokana na pingamizi alilowekewa.
Kata ambazo chama chama che ACT Wazalendo imesimamisha wagombea katika kata mbalimbali ikiwemo Isagahe,iliyopo Kahama mkoani Shinyanga,Kijichi, iliyopo Temeke jijini Dar esSalaam, Nkome iliyopo Mkoani Geita,Tanga iliyopo mkoani Ruvuma na Ihumwa iliyopo mkoani Dodoma.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.